Mahojiano ya Bibi Mwingereza aliyeingia kwenye Ushia kuhusu Imam Hussein (as)

Dk. Rebecca Masterton, Mshia mwenye makazi yake nchini Uingereza ambaye ni Mwislamu mpya, anasema kwamba anajivunia kusilimu pamoja na kufahamu kua Imamu Husein (a.s.)  ni kielelezo cha nafsi safi, tukufu na yenye upeo mkubwa gizani ambao ni nadra sana kwa watu wengi.

Kuhusiana na hilo, anasema:

Imamu Husein (AS) ni mtu anayeheshimiwa na watu wengi duniani kote, kwa sababu watu wanatamani sana viongozi wanaoweza kuwategemea, wale ambao ni mashujaa na wenye mioyo safi, na daima kuna wachache  wao waliopo duniani.

Mtafiti huyu mpya wa Kiislamu wa Kiingereza, ambaye amezungumza kuhusu masuala ya kidini na kiutamaduni kwenye televisheni ya Uingereza na vyombo vingine vya habari, alisema: Imam Hussein (AS) ananitia hamasa kuendelea kutafuta elimu.

Mwandishi wa kitabu cha “Shia Spirituality for the 21st Century” aliongeza: Niliposilimu, sikujua chochote kuhusu Imamu Husein (AS) na matukio ya Karbala, na kumfahamu kwangu Imam ilikuwa ni ufahamu wa taratibu.

Dk. ‘’Rebecca Masterton’’ alisema: Nilipowaona wapenzi wa Ahlul-Bayt (SAW), nilitambua kwamba wao ndio waliokuwa wakihifadhi kumbukumbu na maelezo ya tukio la Karbala na siku ya Ashura, vinginevyo ingesahaulika, na leo tungekuwa na utamaduni tofauti sana wa Kiislamu.

Mwislamu huyo mpya wa Kiingereza aliongeza: Tunaona kwamba tangu wakati wa tukio la Karbala hadi sasa, kuna baadhi ya watu wanatumia dini kwa ajili ya maslahi ya kidunia kama Imam Husein[as] alivyosema.

Dk. Rebecca Masterton alibainisha kuwa jamii bado zinahitaji mageuzi;  Wasema ukweli bado wanauawa na dhuluma bado imeenea.

Credit: Shabestan