ILIKUAJE SHEIKH ZAKZAKY AKAWA SHIA?

Enzi za uwanafunzi wa kiongozi wa Kishia wa Nigeria zilisadifiana na ushindi wa Mapinduzi ya jamuhuri ya Kiislamu  ya nchi ya Iran; Hii ni pamoja na kuwa alibadilika kuwa Shia chini ya ushawishi wa fikra za Imam Khomeini na kuwashawishi Waislamu wa Nigeria kuwakabili Wazayuni.

Kwa mujibu wa kituo cha habari cha Istibsar, Sheikh Ibrahim Zakzaky, ambaye alizaliwa mwaka 1953, ni kiongozi ambaye ni maarufu sana

nchini Nigeria, na mbali na Mashia, MaSunni na Wakristo wa nchi hii, pia wana mapenzi maalum kwake na kumfuata, kiongozi wa Mashia. Kiongozi wa mashia  Nigeria Mwishoni mwa miaka ya 1970, alikua katika maisha yake ya uwanafunzi wakati huo huo wa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran, na maendeleo haya muhimu yalikuwa na taathira kubwa sana kwake.

Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria ni mhitimu wa masomo ya uchumi na alifungwa jela mara kadhaa katika miaka ya 80 na 90. Alihuisha Siku ya Quds nchini Nigeria na sera hii ilipelekea kuuawa kishahidi kwa wanawe watatu kupitia polisi wa Nigeria katika maandamano ya Siku ya Quds ya mwaka 2014. Sheikh Zakzaky alianza shughuli zake katika miaka ya 1980, na katika kipindi hiki, takriban Wanigeria milioni 12 wamekuwa Mashia, na hii imesababisha mashambulizi makali ya baadhi ya makundi yenye itikadi kali dhidi yake.

Riwaya ya Sheikh Zakzaky jinsi alivyokuwa Mshia

Katika moja ya mahojiano yake kuhusu namna alivyokuja kuwa Shia na kuwaalika Waislamu wa nchi hii katika madhehebu ya Kishia, Ibrahim Zakzaky alisema: katika kipindi cha Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, niliona picha na habari hasa kutoka vyombo vya habari vya Magharibi, za matukio ya nchi hii. Tulikuwa tunajishughulisha na shughuli za Kiislamu katika chuo kikuu na tukaunda shirika liitwalo “Islamic Association of Surah Nigeria” ambalo nilikuwa katibu mkuu wake. Mwishoni mwa miaka ya 70, pia nikawa makamu wa rais wa masuala ya kimataifa wa jumuiya hii na mwaka 1980 Nilikuja Iran katika kumbukumbu ya mwaka wa kwanza wa Mapinduzi ya Kiislamu.

Sheikh Zakzaky, kiongozi wa Mashia wa Nigeria

Aliongeza kuwa kabla ya kuja Iran, nilikuwa nikifanya shughuli kama Muislamu na nilitamani kuwa na nchi ya Kiislamu, kuwa na uwezo wa kuchukua udhibiti wa nchi yetu: kwa sababu serikali yetu ilikuwa ya kikomunisti, lakini baada ya kutembelea Iran, maoni yangu yote yalibadilika.Lakini tulihitaji mfano wa kiongozi wa Irani na mafundisho ya Imam Khomeini (RA). Alhamdulillah, harakati za Kiislamu zilianza Nigeria katika miaka ya 80. Harakati hii ilitenganishwa na Jumuiya ya Kiislamu ya Surah, na walikuwa na jukumu la kuleta Jumuiya ulimwenguni.

Zakzaky alisisitiza kuwa: hatukuzungumza kuhusu Mashia au Masunni katika kongamano hili na tulisema sisi ni Waislamu, lakini mwishoni mwa miaka ya 80, serikali na baadhi ya watu walianza kutushambulia na kusema kuwa ‘’nyinyi ni Mashia’’. Hatukuweza kusema kua sisi si Mashia.  Wao walisema nyinyi ni Mashia na mnaamini kuwa Uislamu wenu ni tofauti na wetu.Sisi tunajua kua waislamu wote ni wamoja,  lakini nyinyi mnasema kuwa nyinyi ni tofauti.Kila tulivyojaribu kuwaeleza kua sisi ni mashia na nyinyi ni masuni lakini hata hivyo sisi wote ni waislamu na tunaikubali Imani ya kiislamu, lakini hawakukubali maneno yetu na bado wao walisisitiza kuwa sisi ni watu tofauti.

Kiongozi huyo wa Kishia wa Nigeria alisema: kuwa watu wa Nigeria wanafuata madhehebu ya Maliki. Nilisoma Uislamu katika chuo cha mtaani ambacho ni cha madhehebu ya Maliki, na tulisoma vitabu mbalimbali pale. Baada ya masomo hayo, kuufahamu na kusoma ushia kwangu ilikua rahisi.

Je! Watoto watatu wa Zakzaky waliuwawaje kishahidi?

Mwenendo uliokua wa idadi ya Washia nchini Nigeria na idadi inayoongezeka Umaarufu na mapenzi kwa Sheikh Zakzaky, hisia za chuki za Wazayuni na Uwahabi nazo zikaongezeka, hilo likasababisha harakati za kupambana na Mashia kuzidi kuongezeka hapa nchini. Katika Siku ya Quds mwaka 2014, Mashia na Masunni wengi nchini Nigeria walimfuata Sheikh Ibrahim Zakzaky kuandamana katika barabara za nchi hii wakipinga vitendo vya uadui vya Wazayuni wa Ghaza, ambayo ilikabiliwa na upinzani na nguvu  za jeshi la nchi hii.

Katika maandamano haya, hata kulitokea mzozo kati ya vikosi vya jeshi na Waislamu wa Nigeria, ambao ulisababisha vifo vya zaidi ya wanaume na wanawake wa Kiislamu 30 waliokuwa katika swaum huko Zaria. Wakati huo huo, Nigeria inahusika katika baadhi ya mashambulizi ya kigaidi na shughuli kubwa zinazofanywa na Mawahabi, Kulikuwa na vikundi vya kitakfiri pia. katika Siku ya Quds mwaka huo, watoto watatu wa Sheikh Ibrahim Zakzaky walikuwa miongoni mwa waandamanaji. Na Waliuawa kishahidi katika makabiliano na polisi wa Nigeria.

Maombolezo ya Mashia nchini Nigeria na vilevile maandamano dhidi ya utawala wa Kizayuni katika Siku ya Quds yalikuwa tulivu mno na mbali na anga ya upinzani, lakini kwa vile mtiririko huo ni shwari na unaowiana na mantiki na taathira zake, watu walitambua kuwa uhalali wa kuwepo kwake. Uislamu ndio silaha kuu ya ushindi.

Credit: Estebsar