Kwa mtazamo wa Imam Swadiq (AS), ni zipi sifa za “Muumini”?


Jibu fupi: Imamu Swadiq (a.s.) anaeleza sifa tano za Muumini: Usafi katika kazi na biashara,

tabia njema, usafi wa nafsi(roho), kujitolea katika njia ya Mwenyezi Mungu, na kuzungumza maneno machache, hizi ni katika sifa za muumini.

Jibu la upanda:

قَالَ الإمامُ الصَّادِقُ ( عليه السلام): «المُؤْمِنُ مَنْ طَابَ مَكْسَبَهُ وَ حَسُنَتْ خَلِيقَتُهُ وَ صَحَّتْ سَرِيرَتُهُ وَ أَنْفَقَ الفَضْلَ مِنْ مَالِهِ وَ أَمْسَكَ الفَضْلَ مِنْ كَلامِهِ» (۱)؛

Imamu Swadiq (as) anasema: Muumini ni mtu ambaye kazi na biashara yake ni safi na nadhifu, maadili na tabia yake ni nzuri, na nia na makusudio yake ya ndani na nje ni sahihi, na kama ana ziada kwenye mahitaji ya maisha yake, hutoa kwa wengine, na hunyamaza kuongea maneno ya ziada. Maelezo ya Hadithi: Kudai kua na imani ni rahisi sana, lakini kufikia ukweli wake ni vigumu sana. Katika riwaya hii ya Imam (as), anaelezea sifa tano (5) za muumini:

1. Usafi katika kazi au biashara Mwanadamu anapaswa kutambua mapato yake yanatoka wapi? Je ni ya halali au haramu? Wapo wengi wanaodai kua wanaamini; Lakini njia zao za maisha zinatia shaka. Katika wakati wetu huu, kuna baadhi ya watu ambao Wanadai kua na imani; Lakini mwisho wa siku wanapandisha bidhaa bei masokoni na kuwafanya watu wateseke, ili kupata mapato na faida zaidi, Hicho si kipato halali au katika mambo yanayohusiana Na urithi, kuwanyima urithi mabinti au kinamama, ambapo mambo haya yalikua katika zama za ujahiliya(ujinga) au katika fedha zinazoitwa Qardhul -Hasana walizofanya kwa riba ya asilimia 28% au 30%, hali ya kua faida inatakiwa kua angalau asilimia 2% na ikiwa zaidi ya hapo ni riba. Au wanaanzisha na kuunda taasisi kama vile Goldquist; hali ya kua hio ni moja ya utapeli wa wazi.

2. Tabia njema Maadili na tabia ya Muumini ni nzuri, na anatenda mazuri kwa mke wake, mwanawe, jirani yake, rafiki yake, adui n.k hua na tabia njema, na akiamrisha mema na kukataza maovu au pia kuwaongoza wajinga, basi ni kwa ulimi na kauli nzuri.

3. Usafi wa ndani ya(roho/moyo) Tabia njema ya muumini si ya kubuni; Nje na ndani yake ni sawa(dhahiri na batini), na moyoni pia ni mfadhili na kupendelea watu mazuri. Roho yake ni safi na hana wivu(husda) na wala si bahili.

4. Kutoa katika njia ya Mwenyezi Mungu.

Muumini hutoa ziada ya mali yake katika njia ya Mwenyezi Mungu. Wapo wanaokusanya mali zao na bila ya kuzitumia, wanaziweka tu mali hizo kwa ajili ya wanaobakia, na Siku ya Kiyama hawana budi kujibu maswali kuhusu l mali hizo; hali ya kua hawakunufaika na mali hiyo. Ikumbukwe kwamba mtu anapotoa, humfikia Mwenyezi Mungu kwanza. Watu wengine mwaka mpya wananunua upya vifaa vyote vya nyumbani, wakati watu wengine wanajutia, je Ikiwa ni mtu ana dhamira njema atafanya mambo kama hayo?

5. Sio mzungumzaji sana Muumini haongei sana, Bahati mbaya ya Mwanadamu iko kwenye kuongea kupita kiasi na maneno mengi; Kwa sababu inajenga uadui na kumfanya mwanadamu amsahau Mwenyezi Mungu na kwa sababu hiyo mwanadamu anaingia motoni. Riwaya hii ni muongozo wenye vipengele vitano ambavyo ni nzuri sana vikitekelezwa. Sisi ni wenye utamaduni tajiri na wenye nguvu.

——

1- Usul kafi: J3, Uk. 331