Ikiwa mtu anapata mafanikio kwa jitihada zake, je, anapaswa kusema kua mafanikio hayo ni kwa msaada wa Mwenyezi Mungu?!

Swali:

Salam Alaikum, vile baadhi ya watu wanavyosema, mtu akijitahidi atafanikiwa, na wanavyosema ukijitahidi Mungu atakusaidia pia. Swali hili linakuja kwamba wakati mtu anajitahidi kufanya kitu, anafanikiwa, na haitaji msaada wa Mungu, kwa hivyo msaada wa Mungu una maana gani?!

Jibu kwa ufupi:

Ni sheria, kanuni ya

kimungu kwamba juhudi za kibinadamu zitakuwa na matokeo muhimu sana juu ya mafanikio na natija yao; Lakini kwa upande mwengine, watu wengi wanaweza kua na juhudi, lakini bado wasifikie mafanikio wanayotaka; Kwa sababu mambo na nyenzo ambazo ni muhimu ili kufikia matokeo yenye mafanikio yote hazipo mikononi mwa wanadamu. Katika maono ya kuamini Mungu mmoja, nia, kazi na juhudi za wanadamu vyote ni hiari na uwezo wa Mungu na hapo mwanadamu hawezi kitu chochote. Bila uwezo wa Mungu, mwanadamu hawezi hata kunyanyuka alipo na kujaribu kufanya kitu na ikiwa atajaribu Kama Mungu hajaweka mapenzi yake katika mafanikio yake basi hawezi kupata mafanikio. Kwa kifupi, mwanadamu hana uwezo yeye mwenyewe. Mungu yuleyule aliyemuumba mwanadamu alimlazimisha kufanya jitihada na kujaribu. Na kumpa mafanikio katika juhudi yake.

Na hayo mafanikio anayopata mwanadamu pia ni Mwenyezi Mungu ndie ameyaumba. Kwa maelezo zaidi na kwa mfano, tunasema kwamba: Mungu anaumba na mwanadamu pia hufanya jambo fulani; Lakini kuna tofauti katika aina hizi mbili za ubunifu. Kwa sababu, kwanza kabisa;, ni Mungu pekee aliyeumba nyenzo ya kwanza ya msingi ya uumbaji, na ikiwa mwanadamu anaumba kitu ni Kwa kutumia nyenzo hizo tu. Pili;, uumbaji na uvumbuzi huo wa mwanadamu unawezekana tu ikiwa Mungu ameruhusu; yani kwamba, bila ruhusa na msaada wa Mungu, hakuna mtu mwenye uwezo wa kufanya chochote, na kila kitu kinachotokea sio nje ya mzunguko wa ruhusa ya Mwenyezi Mungu. Kwa tafsiri ya kielimu, mambo na vitendo vinavyotendeka ima ni “asilia” au ” makusudi”. Vitendo ambavyo hutokea kwa kujitegemea na bila msaada wa mtu huitwa “asilia” na vitenzi kama hivyo hutolewa na Mungu tu; Lakini vitendo vinavyotokea bila kujitegemea na kuitwa “makusudi”, hutokea kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, pia imetokea kutoka kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu; yaani viumbe wengine wasiokuwa Mungu, wakiwemo wanadamu, malaika, majini na… Wote Wanafanya mambo kwa idhini ya Mwenyezi Mungu.

Kwa hivyo, ikiwa mwanadamu anaweza kujitegemea kuunda kiumbe bila kuchukua fursa ya muongozo wa uumbaji wa Mungu na bila kutumia vyanzo vyake na bila idhini na mapenzi ya Mungu, anaweza kusimama mbele ya Mungu na kudai kwamba msaada wa Mungu haukuwa na nafasi katika mafanikio yangu, na kwamba nilifikia mafanikii haya kwa juhudi zangu tu; Lakini kutokana na ukweli kwamba hakuna kuimbe yoyote mwenye uwezo huo isipokuwa Mungu, hakuna muumba wa kujitegemea na muumbaji halisi isipokua Mungu; Kwa hivyo, katika ulimwengu huu, hakuna kitu kinachozidi uwezo wa Mungu ili kiweze kutenda kwa kujitegemea bila uwezo wa Mungu na kupata mafanikio.