Zainab Kubraa (sa) katika hotuba ya Mustabsirin

Katika siku ya kuzaliwa Bibi Zainab (sa), ni vyema kujua na kujifunza kutokana na athari za bibi huyu mkubwa na mtukufu katika maisha ya wenye utambuzi, hususan wanawake waliokua mustabsirin.

Amy Hodgkins anasema kuhusu ushawishi wa Bibi Zainab katika maisha yake:

Lakini kitu kilichonivutia sana ni kwamba Bibi Zainab (sa) aliswali sala yake ya usiku hata katika usiku wa 11 wa Muharram.  Sala hiyo

haikuwa sala ya faradhi.  Lakini alifanya hivyo na hakulalamika kamwe kwa Mungu katika nyakati hizo ngumu!  Na hili lilinifanya kuelewa kwamba mambo mabaya yaliyotokea katika maisha yangu hayakuwa kazi ya Mungu, bali ni kazi ya mwanadamu.  Iwapo mtu yeyote anapaswa kulaumiwa kwa matukio hayo, sio Allah Subhana wa Ta’ala.  Mwenyezi Mungu daima amekuwa upande wangu na siku zote alitaka niwapate Ahlul-Bayt. Baada ya hapo ilinibidi kuwa Shia.  Pia niliamua kujichagulia jina la kiShia na nikachagua jina la Zainab.  Sio tu kwa sababu ya uhusiano wa kihisia, lakini pia kwa matumaini ya kwamba nitakuwa na msaada kwa Imam Mahdi (A.S.) kama vile Bibi Zainab alivyokuwa kwa ajili ya Imam Husein.