Nini maana ya “Uadilifu kwenye Kauli”?

Swali:

Nini maana ya “Uadilifu kwenye Kauli”?

Jibu fupi:

“Uadilifu kwenye Kauli” ni kinyume cha kugombana na kubishana, ambayo ina maana ya uadilifu na haki katika hali zote. Bila shaka,

uadilifu unaosifiwa mara kwa mara katika Hadith za Kiislamu, maana yake ni kuangalia kwa usawa maslahi ya binafsi na ya wengine. Ambayo Moja ya matawi ya uadilifu huo ni, uadilifu kwenye kauli. Imam Swadiq (a.s.) alizingatia uadilifu kua miongoni mwa amali njema sana. Na kwamba, nyumba za peponi ni malipo ya wanaofanya uadilifu na kuacha kubishana, kugombana.

Jibu la kina:

Uadilifu katika mjadala, uadilifu ni kinyume cha kubisha na kugombana, Ina maana kwamba mtu anapaswa kuangalia maneno ya wengine kama vile anavyoona maneno yake mwenyewe na kuyatetea sawa na vile anavyotetea maneno yake mwenyewe, kwa maana nyengine awe muadilifu kwa kila mtu na kila sehemu, hata kama mzungumzaji wa maneno hayo ni mtu wa kawaida bali yeye ni msomi mkubwa na maarufu; Hata kama ni mtoto au kafiri na mwenye kudhulumu akisema kweli, basi na aikubali. Japo kua uadilifu ambao unasifiwa sana katika Hadith za Kiislamu unamaanisha kuangalia usawa maslahi ya mtu mwenyewe na ya wengine, lakini moja ya matawi yake ni uadilifu kwenye maneno, kauli. Imamu Sadiq (as) katika hadithi Maarufu anasema:

«سَيِّدُ الأَعْمَالِ ثَلاثَةٌ: إِنْصافُ النَّاسِ مِنْ نَفْسِكَ حَتَّى لَا تَرْضَى بِشَيء إِلَّا رَضِيتَ لَهُمْ مِثْلَهُ وَ مُواسَاتُكَ الأَخَ فِي الْمَالِ وَ ذِكْرُ اللهِ عَلى كُلِ حال “(۱)؛

“Matendo bora ni mambo matatu: kuwa na uadilifu kwa watu kutoka moyoni kiasi kwamba huridhika na kitu chochote isipokuwa kile unachokiridhia kwa ajili yao pia. Na ndugu yake katika dini, kwenye mali na kumkumbuka Mwenyezi Mungu katika kila hali.”

Cha ajabu ni kwamba, katika baadhi ya hadithi tunaona kwamba Imamu Swadiq (as) anapotoa dhmana ya nyumba nne za pepo dhidi ya vitendo vinne, anaona kuacha kubisha kama kitendo cha tatu na kutenda haki kwa watu ni kitendo cha nne, ambapo inaweza kuwa ni uadilifu au haki kwenye maneno au kauli. (2)

1- Al Kafi: J2, Uk 144

2- Akhlaq Fil Qur’an: J2, Uk 293

 

Credit: Makarem.ir