Bingwa Mwanamke wa kunyanyua uzito amekua Muislamu

Tehran, Irena Rebecca Koha, bingwa wa dunia wa kunyanyua vizito kwa wanawake kutoka Latvia, anaonyesha mwelekeo wake wa kidini ya kiislamu kwenye

ukurasa wake mtandaoni.

Rebekah Koha, mnyanyua uzito kutoka Latvia, alitangaza kusilimu kwake na kuwa Muislamu kwenye ukurasa wake wa kibinafsi wa Instagram na kuandika: “Nilifanya uamuzi mkubwa maishani mwangu. Ninaweza kusema jinsi ninavyofurahi na kushukuru.Nina Imani ya kwamba nimefanya maamuzi sahihi. Jambo pekee hilo Ninaomba kila mtu aheshimu uamuzi huu.

Aliongezea: “Ikiwa huna la kusema, unaweza kuondoka kwenye ukurasa wangu na ni bora kukaa kimya.” Leo ndio siku muhimu kwangu kwa sababu nimekuwa Muislamu.

Koha aliendelea: Saa 3:48 mchana, nilitoa shahada na kuwa Mwislamu. Najua kuanzia sasa nimeanza ukurasa mpya na mzuri zaidi wa maisha yangu.Kuanzia sasa nimekua muislamu na nawaombeni kutosambaza  picha zangu za bila hijabu kwenye mitandao ya kijamii.Asanteni Kwa wale wote waliokuwa upande wangu na kuniunga mkono.

Koha alianza kunyanyua mizani akiwa na umri wa miaka 12 na masaa 18 kwa wiki Anafanya mazoezi na mara mbili kwa siku. Pia alijiendeleza katika kazi ya mpira wa vikapu, ngumi na tenisi. Yeye ndiye mmiliki wa dhahabu tatu na fedha moja kwa Watu wazima wa Ulaya na shaba 2 za vijana wa Ulaya, shaba ya Olimpiki ya Vijana ya 2014.Kwa Vijana fedha na dhahabu tatu na shaba 2 katika ubingwa wa dunia na kushinda taji Yeye ni wa nne katika Olimpiki ya Rio 2016.