Kibatu cha Al-Mawsu’a Al kubra Al Mustabsirin

Muhtasari wa yaliyomo katika kitabu hiki:

Katika kitabu hiki, mwandishi amezungumzia mada ya Tawhidi kwa mtazamo wa Ahlul-Bayt (as) na amemtambulisha msomaji juu ya tawhidi ya Kishia kwa kutumia aya na hadithi kwa njia rahisi. Mbali na mada za tawhidi, pia amezungumzia masuala ya sasa ya umma wa Kiislamu.

– Shughuli nyingine muhimu ya Kituo cha Ulimwengu cha Mustabsirin,

kama ilivyotajwa, ni uundaji wa mzunguko mkubwa wa elimu ya Mustabsirin” (tangu mwanzo wa karne ya kwanza ya Hijria hadi karne ya kumi na nne) katika muundo maalum na kwa lugha ya Kiarabu. Juzuu[sehemu] ya kwanza ya kitabu hiki ilichapishwa na kusambazwa muda fulani uliopita, na yaliyomo ndani yake ni pamoja na maelezo ya mchakato wa kufanya kazi katika  kueneza elimu hii, maelezo ya mukhtasari wa imani ya madhehebu ya Shia  ya maimamu kumi na mbili, na wasifu wa kielimu wa wanazuoni wa karne ya kwanza na ya pili ya Hijria.

 

Al-Mawsu’a Al kubra Al mustabsirin

Katika mzunguko huu wa elimu, majina ya watu wote walioacha Uislamu au Ushia baada ya kifo cha Mtume wa Uislamu [saww) kisha wakawa waumini tena, au watu ambao hawakuwa Mashia au hata Waislamu mwanzoni na kishakuwa Waongofu wa Ushia wametajwa na kisha kila mmoja wao kufanyiwa utafiti na kuchunguzwa kwa kina.  Kwa mfano, tunaweza kutaja watu wakubwa katika historia kama vile: Har bin Yazid Riyahi, Zuhair bin Qain, Zurara na wengine waliobadilika.

Kumbuka: Majina ya waongofu hawa wote wa Shia yametajwa kwa mpangilio wa karne walizoishi.

Muhtasari wa mchakato wa kuandaa mzunguko wa taaluma kuu ya Mustabsirin

Utaratibu (wa hatua hizi) ni ifuatavyo:

  1. Kutaja jina, ukoo na cheo cha Mustabsir.
  2. Kutaja tarehe ya kuzaliwa na kufa au kuuawa kishahidi mustabsir.
  3. Kutaja mahali alipo kuzaliwa na mahali alipo kulia na maendeleo ya Mustabsir.

Pia, mambo kama vile: Jihad na vita alivyoshiriki na Mustabsir, mazungumzo na maoni ya Mustabsir, maoni ya wengine kuhusu kila Mustabsir iwe kutoka kwa marafiki zake na majirani au watu walioishi katika zama zake, nafasi yake ya kijamii, kielimu na kisiasa Na… Mustabsir , Huduma za Mustabsir na maudhui mengine muhimu yatatajwa.

  1. Simulizi za hatua za mabadiliko ya kiakili na utambuzi.
  2. Maneno ya wengine kuhusu Mustabsir.
  3. Kutaja vitabu na kazi za mustabsir katika nyanja mbalimbali: kielimu, kitamaduni, kijamii, kisiasa, nk.
  4. Kutaja vitabu na makala zilizoandikwa kuhusu Mustabsir.
  5. Kutaja majina ya vitabu ambavyo wasifu wa Maisha ya Mustabsir umetajwa au vitabu ambavyo sehemu ya wasifu wa Mustabasr imetajwa.  Isifichwe kwamba kutajwa kwa vyanzo hivi ni kutoka katika vitabu tofauti vya (Shia na Sunni).
  6. Kutaja Hadith kuhusu Mustabsir kutoka kwa Ahlul-Bayt watakatifu na wasafi (as). Katika Hadith hizi, anaweza kuwa ametukuzwa au hata kulaaniwa (kabla ya Istibsar).  (Sehemu hii inahusiana na mustabsirin walioishi katika zama za Ahlul-Bayt, [as], yaani kabla ya ghaiba kubwa, ambao wanajulikana kama waanzilishi, kama vile: Zurara b’Ayn, Hisham ibn al-Hakam, na kadhalika.)