Mazungumzo na kijana wa Canada aliyesilimu mwezi wa Ramadhani – Subhanallah

Gregory Soden anaamini kwamba: “Katika nchi zote za Magharibi Watu wengi hawana Imani za  kiroho na watu wengi wanaenda Kuitafuta. Inaonekana  falsafa za Mashariki kuwa kawaida sana na kusababisha watu wengi wanaotafuta Imani ya kiroho kwenda upande huo, lakini si wote wanaoamini Mungu mmoja. Nchini Canada, kuna Idadi kubwa ya watu ambao

wamebadili dini na kusilimu.Ikiwa tunaweza kujenga mahusiano na vijana kwa njia ambayo wao  inawavutia basi tunaweza kuongeza Uislamu, kwa hiyo kuna pengo ambalo linaweza Kujazwa na Uislamu.”

Gregory Sudan, kwa jina la Kiislamu la Ali Mahdi, ni kijana Mshia kutoka Canada ambaye zamani alikuwa Mkristo Mkatoliki. Wakati wa mazungumzo na ukurasa wa Kiingereza,wa Shafaqna alisimulia hadithi ya safari yake kutoka Ukristo hadi Uislamu na akachunguza wasifu wake Pamoja na Vijana Waislamu wapya katika nchi za Magharibi.

Jina langu ni Sudan na nilijichagulia jina la Kiislamu Ali Mahdi, ingawa katika Uislamu jina la mtu likiwa na maana nzuri hakuna haja ya kulibadilisha, hivyo Gregory Sudan bado ni jina langu halali, Familia yangu na marafiki wananiita Greg na pia Ali Mehdi. Nililelewa kwenye shamba la kufungia  ng’ombe na kuku wa nyama katika Norfolk, Ontario, Canada. Mama yangu alinilea kama Mkatoliki wa Roma.Baba yangu ni protestani[nae yupo katika umoja wa makanisa ya Canada] Pande zote mbili za familia yangu ni za kidini, mama yangu ndiye mlezi aliyetufundisha mambo ya dini.

 

Nilisilimu tarehe 15 mwezi wa 12 mwaka 2001 nikiwa na umri wa miaka 16, yaani nilipokuwa nasoma shule ya sekondari ya Roma katoliki katika mji mdogo ambao bila shaka hakukuwa na muislamu yoyote, Wakati huo sikumjua mtu yoyote muislamu na nilifanya mawasiliano na  Waislamu online tu.

Je!Unaweza kutuambia kuhusu masomo yako ya Kiislamu na kitaaluma[chuo]?

Nina shahada ya kwanza katika historia ya umma kutoka Chuo Kikuu cha Wilfred Laurel huko Waterloo, Ontario na nimekuwa nikiishi Qom tangu mwaka 2010 na kusoma katika Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al-Mustwafa (RA).Na kwa sasa niko mwishoni kupata shahada yangu katika mafunzo ya ushia katika chuo kikuu cha Imam Khomeini katika chuo kikuu cha kimataifa huko Al-Mustwafa.

Uliujuaje Uislamu? Kwa nini umechagua mafunzo ya uShia?

Kabla sijasilimu nilienda kanisani kila wiki na sikuwahi kuhoji imani yangu kwa sababu sikujua tofauti yoyote. Ninaapa kwamba nilikuwa Mkatoliki mwaminifu, Alisema kwamba kila muda mtu alipoongelea vibaya madhehebu ya katoliki, nilikuwa nikijaribu kuthibitisha kwamba maneno yao hayakuwa sahihi, ingawa sasa najua hilo, wakati huo[elimu] Ujuzi wangu ulikuwa mdogo.

 

Nilipoanza kutafiti Uislamu, sikutaka kuukubali. Nilisoma tu kuhusu Uislamu kwa sababu ya kupendezwa na masomo, lakini polepole niliipenda, nilipenda kujifunza kuhusu dini na tamaduni tofauti nilipokua kijana. Babu yangu mzazi wa baba alikuwa na mkusanyiko mkubwa wa magazeti ya National Geographic yaliyoanzia miaka ya 1930, pamoja na idadi kubwa ya magazeti mengine kutoka nchi mbalimbali yaliyonivutia. Pia nilianza kusoma vitabu vya jografia ambapo nilipata shauku kubwa katika jiografia na imeunda matukio na historia ya sasa.

Kuishi katika mji mdogo ambapo hakukuwa na watu wasio Wakristo kulinifanya niwe na hamu ya kutaka kujua ulimwengu wa nje. 96% ya watu katika mji wangu ni weupe, na si kawaida kuona watu wa rangi tofauti isipokuwa watu weusi na Wachina katika mji huu. Tuliona watu wachache wa kikabila na kidini  katika miji mikubwa tu kwa sababu huko Canada mara nyingi watu  hawaishi katika miji midogo.

Kulingana na utafiti wa watu ambao walibadilisha dini ni jitihada zao za kiroho au mgogoro wa kibinafsi Waliopata, lakini mimi sikuwa kama hivi. Nilikua mtu wa kidini na sikuwahi kunywa pombe wala kutumia dawa za kulevya bali Nilipenda kufanya utafiti tu.

 

Mwaka wa 2000 nilikuwa nikitafuta watu kutoka nchi mbalimbali wa kuzungumza nao mtandaoni kwa sababu nilipenda kujifunza kuhusu watu tofauti. Katika miaka kabla ya kuenea kwa mitandao ya kijamii kwenye wavuti Nilijiunga na tovuti ya urafiki wa mawasiliano na kijana Yahya ambaye ni kijana Alikuwa Muislamu wa Kishia kutoka Kuwait Tuliwasiliana kupitia email na Messenger na hadi sasa tunawasiliana.

 

Nilimuuliza juu ya dini yake kwa sababu sikujua kitu juu yake, hata hivyo sikuwahi kufikiria kusilimu kwa sababu nilifikiri kuwa nina faraja kuwa Mkatoliki. Nilipokua sekondari nilisoma kozi ya ‘’ DINI ZA ULIMWENGUNI’’, nikaona mapenzi yangu kuzidi katika dini ya Uislamu. Katika Vitabu vyetu vya masomo, vilikuwa na habari kuhusu nafasi ya yesu Kristo (SA) katika Uislamu. Ambayo inaweza kuonekana katika Qurani pia.Nilijua kwamba yesu Kristo ni nabii aliyekubalika katika Uislamu, lakini sikujua umuhimu wake katika Uislamu. Pia, sikujua kuwa mama yake Bibi Maryam (SAW) Anajulikana kama mmoja wa wanawake wanne watukufu wa Uislamu!.

Siku hiyo baada ya shule, niliporudi nyumbani, nilichunguza mtandaoni nafasi ya yesu Kristo katika Uislamu. Pia nilikuta baadhi ya vitabu katika maktaba ya shule kuhusu Uislamu, lakini mada zao zilikuwa za ujumla sana, kwa sababu shule yetu ya sekondari ilikuwa shule ya Kikatoliki. kwa sababu ya ukosefu wa upatikanaji wa vitabu kuhusu Uislamu na bila kuwafahamu Waislamu wowote karibu nilitegemea mtandao kujifunza zaidi kuhusu Uislamu,baada ya utafiti wa hali ya juu kuhusu nafasi ya yesu kristo katika Uislamu, sikuweza tena kuukubali mtazamo wa Kikristo na Uungu wa Yesu (PBUH) imani ya Kiislamu ilifungua akili yangu kwa ukweli.

Ambako sikuwahi kuwaza kuhusu Ukristo na Yesu (AS) kwa ujumla dini yangu, kwa maelezo niliyosoma, niliamini kuwa Uislamu ni ukweli.Kila nilipokua nikisoma Zaidi kuhusu nabii Issa na itikadi za kiislamu, nilipata shauku Zaidi ya kubadili dini yangu.Kwa utafiti niliofanya nilitambua Zaidi kua Uislamu ndio haki. Hoja zilikuwa nzuri na hata uthibitisho wa utume wa Muhammad (SAW) na Uislamu katika Biblia, Sikuchukua uamuzi huu kirahisi.

Wakati huo huo nilipokuwa nikijifunza zaidi na kuwa mgumu zaidi katika masomo yangu ya Uislamu, nilimtumia barua pepe rafiki yangu wa Kuwait na kumweleza kuhusu matokeo yangu ya masomo. ‘’Nilimwambia kwamba ningehitaji kusilimu nitakapojifunza zaidi kuhusu Uislamu’’. Sikukusudia kufanya hivi kwa haraka kwa sababu kufuata Uislamu katika mji wangu bila kuwa na watu wengine haikuwa kazi rahisi. Niliamua kusilimu nilipokwenda chuo kikuu kwa sababu sikuweza kwenda msikitini hadi wakati huo. Nikamwelezea Yahya Habari hii, yeye Alisema kuwa hakuna haja ya mimi kwenda msikitini na ninaweza kutamka shahada mbili wakati wowote nikiwa tayari na kuswali nyumbani. Mnamo tarehe 15 Disemba 2001{29 Ramadhani 1422} kwa kupitia mtandao wa messenger nilitamka shahada mbili kwake: {Hakuna Mola apasaye kuabudiwa ila Mungu mmoja na Muhammad ni Mtume wake} na kwa kutamka maneno haya mazuri nikasilimi.

Baada ya kuhitimu kutoka shule ya sekondari, karibu mwaka mmoja na nusu baada ya kubadili dini, alianza kusoma historia ya umma katika Chuo Kikuu cha Wilfred Laurier huko Waterloo, Ontario, Canada. Kwa kuishi huko nilipata mahusiano na Waislamu na kwa mara ya kwanza nikashiriki  katika programu hizo na  Nilihudhuria msikitini.Nilifaidika sana kwa sababu ya mihadhara na urafiki na masheikh Shafiq Huda na Salim Bimji.

Tofauti na watu wengi wanaosilimu, mimi nimekuwa Shia tangu mwanzo na nilichagua Ushia wakati huo huo nilipokuwa Mwislamu, Niliposoma kuhusu maisha ya Mtukufu Mtume (SAW) kwa sababu ya shauku yangu kubwa katika historia na marejeo ya mara kwa mara kwa Mtume nilimuona Ali (SAW).Na Hili ndio lilinifanya nisome sehemu za Nahj al-Balaghah na kusoma matukio ya Ghadir Kham na Saqifah. Masomo haya yaliongeza mapenzi yangu kwa Imam Ali (AS) na pia yaliongeza imani yangu kwamba yeye ndiye mrithi wa kweli wa Mtume (SAW).

Ni mabadiliko gani yalitokea katika maisha yako baada ya kusilimu?

Kusilimu kuliniletea matatizo mengi katika familia yangu, hasa kwa mama yangu, ambaye alikuwa mpinzani mkubwa wa kusilimu kwangu. Nilipomwambia mama yangu kuwa nimekuwa Muislamu, alikasirika sana. Hasira zake ziliendelea hadi mwaka wa 2004,baada  ya hapo alikubali suala hilo, ingawa hakua radhi na uamuzi wangu.

Nilipopokea vitabu vya dini kwa njia ya posta, pamoja na Qurani Tukufu, mara baada ya kusilimu kwangu, ilinibidi kuvificha kwa sababu ya mama yangu. Alikasirika sana aliponiona nikisujudu kwa sababu ilikuwa ni ishara ya wazi kabisa kwamba mimi si Mkatoliki tena . Wengi wa wanafamilia yangu wamesema vibaya juu ya kusilimu kwangu, ingawa babu yangu mzaa mama, ambaye alijulikana kwa imani yake, hakupenda kusilimu kwangu. Bibi yangu mzaa mama pia mwenye dini sana na kaka yake ni mmoja wa askofu mstaafu nchini Uingereza kamwe hawakusema chochote juu ya kusilimu kwangu.

Kabla sijaenda chuo kikuu, mama yangu alikuwa akiniusia kua kila wiki  Niende kanisani, Nilikua nikienda kanisani hadi Oktoba mwaka 2003, ambayo inalingana na mwezi wa Ramadhani.

Ilikua vigumu sana kuvunja heshima kwa mama yangu, kwasababu ya kunilazimisha kufanya jambo gumu kwakua nilikua nikifunga swaumu ya Ramadhani,nilikuwa nikiweka mkate wa Ekaristi uliokuwa ukitolewa kanisani kama mkate mtakatifu mfukoni mwangu, lakini mama yangu aligundua na alikuwa na hasira na aibu juu ya hili, na baada ya hapo, sikuula tena. Baada ya hapo Sikuenda tena kanisani isipokuwa mazishi ya babu yangu.

Safari yangu ya Uislamu na maisha yangu kama Muislamu milele Haikuwa rahisi na ilibidi nipigane katika njia hii na kujitolea sana.

Kwa maoni yako Ni ujumbe gani muhimu zaidi wa Uislamu na Quran?

Msisitizo mkubwa wa Uislamu ni juu ya tawhidi na inatufundisha kwamba Mwenyezi Mungu ni mwingi wa rehema, mwenye nguvu na wa kipekee na amewaongoza wanadamu kupitia manabii, akateremsha Kitabu kitukufu na ishara za asili. Mada kuu za Qurani Tukufu ni Mungu, Mitume, Mwanadamu, kitabu kitakatifu, na dhambi. Mwenyezi Mungu ni Mwenye kurehemu, Mwenye kusamehe na zaidi ya yale yaliyomo ardhini na mbinguni. Mwanadamu anaongozwa  na kitabu kitakatifu alichopewa Mtume Muhammad (SAW).

Uislamu na Ukristo vinalingana  nini? Ni Jinsi gani dini hizi mbili kuu zinavyoweza kusaidia ubinadamu kufikia amani endelevu na ya kimataifa?

Ukristo na Uislamu pamoja na Uyahudi ni dini za Ibrahimu na za Mungu mmoja ambazo zote zinaamini katika Mungu mmoja. Zinatofautiana tu katika maelezo. Iwapo Mayahudi, Wakristo na Waislamu wote watafuata dini yao kwa sura safi,sahihi, asilia na isiyopotoshwa, wanaweza kumsaidia mwanadamu kufikia amani iliyotulia na ya kimataifa, lakini kwa hali ilivyo sasa naamini kuwa ni Uislamu wa Shia pekee ambao unamaanisha dini ya kimapinduzi, ambayo inasimama dhidi ya ukandamizaji, inaweza saidia ubinadamu kufikia lengo hili.

Je, unautambulishaje Uislamu kwa WaCanada? Je, una shughuli gani za kidini katika nchi yako?

Kwa sababu jamii ya Canada ni jamii isiyo ya kidini bali ni ya kidunia  na upendeleo na ukweli kwamba WaCanada wengi hata Ukristo hawauzingatii sana na  mafundisho ya Uislamu kwao ni kazi ngumu sana. Bado ni vigumu kwa wengi  wale ambao ni wa kidini. Kuna watu wengi wa kidini lakini  hawana hamu ya kusoma au kuchunguza Dini nyingine.

Ninapenda wazo la kushiriki katika kazi ya watangaza dini, lakini kwa uzoefu na uchunguzi wangu, watu wengi hawapendi kuwasikiliza watangazaji dini. Nimesoma mengi kuhusu Wakristo wa kiinjili  Mashahidi wa Yehova, na Wamormoni ambao wanajishughulisha na kazi ya umishonari. Wakati vikundi hivi vinapojaribu kuhubiri dini yao, wengine wanawaelezea na kuwaona kama “wasumbufu.” Nimesikia kwamba wamisionari wa Ahmadiyya wanaenda nyumba kwa nyumba katika miji na kuwa na mikutano na kutangaza kuhusu Uislamu katika maktaba za mitaa, lakini hawakuzingatiwa sana.

Uislamu unatufundisha kwamba amali ni muhimu. Ikiwa tunaweza kuwasaidia watu wa kipato cha chini kwa kuunda benki za chakula na huduma, kazi hii inaweza kuvutia wasio Waislamu. Kushiriki katika kazi ya madhehebu mbalimbali na kuzungumza kuhusu Uislamu kitaaluma katika makanisa na mashule pia ni njia nzuri ya kuwavutia wasio Waislamu. Kwa uzoefu wangu mimi Wakristo wa kiinjili wana mwelekeo zaidi wa kubadili dini yao kuliko wengine.

La muhimu ni kwamba mtu anaposilimu, hatuwezi kumuacha baada ya kutamka Shahadataini tu. Tumeona kwamba Waislamu wengi wanaiacha dini baada ya kusilimu kwa sababu ya wale waliowasaidia kusilimu kisha wakawaacha. Wengine wanasema kwamba hawawezi kuendana na mazingira ya kikabila na kitamaduni ya misikiti katika jamii za magharibi. Nilishuhudia hili mwenyewe na lilinihuzunisha, lakini namshukuru Mungu imani yangu ilikuwa na nguvu kiasi cha kupuuza matatizo haya na Najua kuwa Uislamu ni zaidi ya utamaduni.

Je, ni changamoto zipi wanazokumbana nazo Mashia nchini Canada?

Sikukulia katika uislamu huko Canada na nilihudhuria tu kituo kidogo cha Kiislamu huko Kitchener nilipokuwa mwanafunzi na kabla ya kuja Qom. Waislamu katika miji mikubwa kama Toronto na Vancouver wana chaguo zaidi katika kila nyanja kuliko watu wanaoishi katika miji midogo kama Kitchener. Wanaweza kupeleka watoto wao shule za kiislamu.

Kwa kadiri nilivyoona na kusoma, vijana wanahitaji kujifunza na kufurahia mambo katika mazingira salama na kulindwa dhidi ya uharibifu na ufisadi katika mazingira na jamii zao. Nimeona vijana wa Kiislamu waliozaliwa na kukulia Canada kwa wazazi wa kidini, wawe wamezaliwa Canada au wenye historia ya uhamiaji, wasiojali umuhimu na kufuata Uislamu au wasioamini tena Uislamu. Kuna vishawishi vingi katika shule za umma,na hata Wakristo wanakumbana na tatizo sawa na hili kwa watoto wao. Shule za Kiislamu ni muhimu ili kuwalinda watoto wetu. Tuna shule chache kati ya hizi za kiislamu na lakini hazipatikani kwa kila mtu kwani nyingi ziko katika maeneo ya miji mikubwa ya mijini kama vile Toronto, Montreal na Vancouver. Na hata uwezekano wa kushirki watu wengi katika shule hizi ni mgumu kwasababu ya tatizo la kifedha.

Mtu anapojiunga na Uislamu, basi si kila kitu kinachofuata hua rahisi, kwa watu wanaosilimu kwa sababu ya kukataliwa na familia zao na kutoonyesha ushirikiano kwa mikusanyiko ya misikiti kwa kukosa ukarimu na wako katika hatari ya kutengwa kijamii na kidini. Watu waliosilimu kwa kawaida Wametengwa na mikusanyiko ya misikiti kwa sababu wao ni wa makabila tofauti. Misikiti mingi nchini Canada inamilikiwa na Waislamu wenye asili ya India, Pakistani, Iraqi, Lebanoni n.k, na watu waliobadili dini hawakubaliwi katika makutano hayo kwa sababu ni wageni. Ikiwa hawata karibishwa misikitini na wakapoteza familia zao, watakuwa wametengwa mara mbili. Kwa hiyo, misikiti katika nchi za magharibi inapaswa kuwa na ukaribu[mapenzi] na kukaribisha kwa sababu Kuwakubali Waislamu wapya ni moja ya wajibu wao.

Je! Kwa maoni yako, ni mada zipi, vitabu na vyombo vya habari kuhusu Ushia vinahitajika kwa Waislamu na wasio Waislamu katika nchi za Magharibi?

Kwa bahati nzuri, vitabu vingi vya Kiislamu vimetafsiriwa kwa Kiingereza, lakini vinahitaji kuboreshwa ubora. Tovuti ya Uislamu ni nyenzo moja bora na yenye lugha nyingi. Kuna vitabu vingi kuhusu mada mbalimbali, lakini bado kuna uhitaji wa vitabu Zaidi kuandikwa au kutafsiriwa.

Kwa bahati mbaya, Waislamu wengi katika nchi za magharibi wanafanya kazi na Hawana muda wa bure wa kujifunza kuhusu Uislamu. Watu wengi kwa Kusikiliza na kushiriki kikamilifu katika mikutano wanajifunza zaidi kuliko kusoma.  kozi za muda mfupi ambazo hufanywa kwenye misikiti au mtandaoni na mashekhe, ambao wamesoma katika seminari[vyuo] zinazojulikana. Hii Ni njia bora ya kufundisha elimu ya Kiislamu kwa Waislamu na inaweza kuvutia watu wengi zaidi.

Podcaste na video kwenye mitandao ya kijamii ni mbinu bora na maarufu ya kueneza mafundisho ya Kiislamu, na kuna mifano mingi ya podcaste na idhaa za YouTube za kufuatilia.

Kwa maoni yako, vijana wa Kanada wako tayari vipi kuukubali Uislamu? Jinsi gani mafundisho ya Kiislamu yanaweza kuboresha maisha yao?

Katika nchi zote za magharibi, ni watu wengi hawana imani ya kiroho, na watu wengi wanaonekana kwenye kuzitafuta Imani hizo.  Inaonekana Falsafa za kiMashariki ni za kawaida sana miongoni mwa wale wanaotafuta imani ya kiroho, lakini si lazima waamini katika Mungu mmoja. Nchini Canada, kuna idadi kubwa ya watu ambao wamebadili dini na kusilimu. Ikiwa tunaweza kuwa na mahusiano nao kwa zile njia zinazowavutia wao, Tunaweza kuwaongoza kuelekea katika Uislamu. Hivyo Kuna kitu au pengo ambalo linaweza kujazwa na Uislamu.

Mafundisho ya Kiislamu yanaongeza ubora wa maisha kwa sababu Uislamu una msimamo thabiti juu ya maadili ya kibinafsi na kijamii. Uislamu unakataza mambo mengi yanayosababisha matatizo na ufisadi katika jamii, yakiwemo pombe, dawa za kulevya, wizi, mwingiliano usio na sababu baina ya jinsia[wake kwa waume], utengano wa familia, machafuko ya kijamii, machafuko ya kisiasa, kujiua, ufukara na mfadhaiko n.k, na uislamu unaweza kusaidia kutatua matatizo yote haya ya kijamii.