(Pichani): Mwanamke kijana wa Kithailand aliekuja kuwa Shia kwenye kaburi tukufu la Imam Ridhaa (a.s)

Mwanamke huyu wa Kithailand alisema kwamba: kila dini na madhehebu niliyojifunza, niliona nyenzo za thamani zimetawanyika, lakini Ushia ndiyo dhehebu ambayo kanuni za kina zaidi zilijadiliwa kwa kina, na Waislamu wanaweza kufika kileleni kwa juhudi katika hali ya kiroho na ukamilifu.

Mwanamke huyu wa Kithailand alisema kwamba: kila dini na madhehebu niliyojifunza, niliona nyenzo za thamani zimetawanyika, lakini Ushia ndiyo dhehebu ambayo kanuni za kina zaidi zilijadiliwa kwa kina, na Waislamu wanaweza kufika kileleni kwa juhudi katika

hali ya kiroho na ukamilifu.

Mwanamke wa dini ya Kibudaa kutoka Thailand akitekeleza ibada ya kutamka shahada mbili za kiislamu  katika kaburi takatifu la Imam Ridhaa[as] na kuwa Mwislamu na akachagua jina la Maryam.

Kwa mujibu wa ripoti ya Ferraro, ikinukuu kutoka mji mtakatifu wa Imam Ridhaa[as], katika sherehe, mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 32 kutoka Thailand, baada ya miaka kadhaa ya utafiti na masomo, ameingia dini ya kiislamu na akachagua dhehebu ya Ushia.

Orayan Roya Miyal alisema: Miaka 11 iliyopita, nilikutana na mfanyakazi mwenzangu ambaye alikuwa Mwislamu, na nilipoona tabia, sala na dua zake, nilipata mwelekeo mkubwa  na kutaka kuelewa dini hii zaidi.

Akaongeza: Nilifanya utafiti na kusoma kuhusu dini na madhehebu mbalimbali kwa miaka mingi na hatimaye, kutokana na kuwepo na mapungufu katika dini hizo, niligundua kuwa Uislamu na Ushia ni dini na dhehebu bora na kamilifu zaidi na nikaamua kuwa Muislamu.

Mwanamke huyu wa Thailand alisema kwamba: kila dini na madhehebu niliyojifunza, nilipata nyenzo za thamani kwa njia iliyotawanyika, lakini Ushia ndiyo dhehebu ambayo kanuni za kina zaidi zilijadiliwa kwa kina na kwa juhudi Waislamu wanaweza kufikia kilele cha kiroho na ukamilifu.

Akisisitiza kwamba sala ni aina nzuri zaidi ya ibada katika Uislamu, Bibi huyu mpya wa Kiislamu alisema kwamba: sala ina nafasi ya juu na muhimu katika dini hii na kwa ujasiri tunaweza kusema kwamba ni ibada maarufu zaidi na inahesabika kuwa ibada bora zaidi ya ibada zingine.

Roya Mayal aliongeza kuwa: eneo la kaburi takatifu la Imam Ridhaa ndio mahali pazuri pa kuanzia kuzaliwa kwangu upya na ninafurahishwa na chaguo hili na ninatumai kupata ukweli wa dini hii na kufikia ukamilifu katika njia hii.

Mwishoni mwa kikao hiki, wasimamizi wa masuala ya mazuari wakigeni wa mji mtakatifu wa Mash had waliwasilisha juzuu ya Neno la Mwenyezi Mungu[Quran] ya kiingereza, mswala, nguo ya kuswalia, vitabu na zawadi za kitamaduni[dini] kwa bibi huyu mpya wa Kiislamu.