Mufti wa Kisunni wa Kifaransa; amekua Shia

Ninajisikitikia kwamba mpaka sasa nina umri wa miaka 68 Sikuujua uShia na nina furaha sana. Kabla ya hili, wakati wa safari yangu ya kwenda Madina, nilifahamu uShia na familia ya Mtume huko Iraq, Lakini leo nimewagundua. Huko madina walituficha kuwafahamu familia ya Mtume[saw] lakini leo

tumegundua hilo.

Sheikh Sanko Mohammadi, Mufti wa Kisunni wa Ufaransa na imamu wa msikiti na mshauri wa masuala ya kidini, baada ya kuzuru Iraq baada na kutembelea tamasha ya kiangazi ya mashahidi na kukutana na Hujjat al-Islam, Walid al-Baaj aliingia kwenye Ushia.

Alisema katika hotuba zake: “Sikuamini kwamba Karbala na Mashia wako hivi. Nilipoamua kuja Karbala, familia yangu ilinizuia sana na kuniambia kuwa, Iraq ni uwanja wa vita, licha ya pingamizi nyingi za kuja Iraq lakini Nilikuja Iraq kufanya utafiti katika uwanja huu.

Aliongeza kwamba: niliufahamu uShia huko Karbala, jambo ambalo sikuwahi kufahamu hapo awali, Niligundua kuwa nilitoka gizani kwenda kwenye nuru na sasa najiona niko huru.

Sheikh Mohammadi alisema kuwa: nasikitika kwa kuwa sikuufahamu uShia hadi sasa, nikiwa na umri wa miaka 68, na ninafurahi sana kuwa mmoja wa askari wa Imam wa zama hizi.

Aliendelea kusema: nilisafiri kwenda Madina kabla ya hapa, lakini sikuufahamu ushia madina kama kiwango ambacho nilikuwa Iraq,  Nilifahamu Shia na Ahlul-Bayt wa Mtume (SAW). Madina ilikuwa imetuficha familia ya Mtume, lakini leo tumegundua hilo.