Kitabu cha Adhwa’at fi twariq Al-haq

Kitabu cha Adhwa’at fi twariq Al-haq kimeandikwa na Mustabasir Mheshimiwa, Bw. Marwan Khalifat.

Muhtasari wa yaliyomo katika kitabu hiki:

Kitabu hiki kiliandikwa na mwandishi na

mustabsir mchambuzi anayeheshimika Bw. Marwan Khalifat.  Maana ya jina la kitabu hiki ni: Jumbe zenye nuru kwenye njia ya uongofu (mtazamo kuelekea hadith za kidini).

Makusudio ya mwandishi katika kuandika kitabu hiki ni, changamoto na mashaka ambayo yametolewa na wapinzani wa Ushia, na Profesa Marwan Khalifat amekabiliana na maswali hayo katika njia ya uwongofu, na kwa dhamiri yake safi, amejibu mashaka haya baada ya utafiti Na uchunguzi wa kina aliofanya, na amechagua dhehebu yenye haki ya Ushia kwa ujasiri wa moyo.