Kitabu cha Fadhl ala Al-A’imat fii hifdh Al’Qur’an wal inayata bihi

Imetungwa na Mheshimiwa Mustabsar, Bw. Marwan Khalifat.

 Muhtasari wa yaliyomo katika kitabu hiki:

Kitabu hiki kiliandikwa na mwandishi na mchambuzi anayeheshimika Bw. Marwan Khalifat. Katika kitabu hiki, mwandishi ameshughulikia mada ya dini ya Qur’ani.

Amethibitisha ukweli huu kwamba Shia ndio bora miongoni mwa Ummah wote katika kuhifadhi, kusoma, kukusanya, kuweka alama katika Qur’ani na kutafasiri Qur’ani Tukufu na hakuna dini yoyote ya Kiislamu iliyoitumikia Qur’ani kwa namna hiyo.