Taasisi ya Imam Hadi (a.s) ilimkaribisha mkuu wa Hawzah Iran, mheshimiwa Ayatollah A’arafi

Mnamo tarehe 26 Shawwal 1445, Taasisi ya Imam Hadi (amani iwe juu yake) ilimkaribisha mkuu wa Hawzah Iran, Mheshimiwa Ayatollah A’arafi.

Katika mkutano huu, Ayatullah A’arafi, alipokuwa akitembelea shughuli za Taasisi ya Mostabserin, alisifu shughuli za wasimamizi wanaoheshimika na watafiti na wafanyakazi wa taasisi hii na kuwatakia mafanikio.

Huku akisisitiza ulazima wa shughuli za kielimu na uenezi katika uwanja wa kutambulisha wale waliokuwa Mashia kwa ulimwengu, haswa watafiti na wasomi, rais mweshimiwa wa Hawzah alibainisha kuwa kitabu “Dairatul Ma’arif Mustabsirin”, ambacho ni moja ya shughuli muhimu za kielimu za hichi kituo, ni utafiti mpana sana na adimu katika uwanja huo tafiti zinalenga kuhudumia chuo  kipana  cha Ahl al-Bayt (amani iwe juu yao)

Kiongozi wa Taasisi Mostabserin,mheshimiwa Hujatul Islam wal Muslimin Sayyed Mirsajadi, huku akimkaribisha Ayatollah A’arafi, alitoa maelezo kuhusiana na shughuli za kituo hiki katika nyanja mbalimbali.