KWENYE MIMBARI YA MWANAZUONI WA KIJAPANI!

Ibrahim Sode Hachaki, mwanazuoni wa Kijapani!

Weblog ya “Bayan”, ambayo mwandishi wake ni mwanafunzi wa Shahada  katika kozi ya biolojia nchini Japani, ilimnukuu

Hujjat-ul-Islam wa Japani na kuandika kwamba inawachukua miaka 40  mpaka Wajapani kufikia hadhi ya kiroho na dini ya Wairani.

Kama mwanablogu huyu alivyoandika, “Hujjat-ul-Islam Sheikh Ibrahim Sawada” alisema kwamba “Mjapani akitaka kufikia hatua ambayo nyinyi [Wairani na Mashia] mlipo, lazima apitishe miaka 30-40 na hio ni kwa neema ya Mungu, miaka 10 lazima  asome Tauhidi.” Anapaswa kusoma na kupata majibu ya mashaka yake, anahitaji miaka 10 mengine ili kuelewa na kuukubali utume wa Mtume Muhammad Mustafa (saww) na miaka 10 kwa kuuelewa Uimamu na…”

” Mimbari ya Hujjat  al-Islam wa Kijapani”

Nikajiwazia, Ewe Mungu, nifanye nini sasa, kwa sala ya mjapani!  Hujja al-Islam wa Kijapani! Bwana “Sheikh Ibrahim Sawada”;  Naam kwasababu, Wajapani wana matatizo katika kutamka maneno ya lugha nyingine, kwa mfano, kamwe hawatofautishi kati ya herufi “l” na “r”, sasa ikiwa matamshi ni mabaya, maombi na sala zetu zitakuwa na shida.

Lakini hapakuwa na njia nyingine, na kwa upande mwingine, kutokana na ukweli kwamba kulikuwa na sifa nyingi sana kwa mtu huyu mwema kiasi kwamba Mungu akamuongoza kwenye njia hii ya nuru na akamjumuisha katika idadi ya marafiki na Mashia wa Ahlul al-Ahlul -Bayt, pia kutoka nchi ya Shinto-Buddhist, nilipenda kuswali nyuma yake kuomba na kuwekeza kwa ajili ya akhera.

Wakati huo huo, tulifunga swafu za swala na akaanza kuswalisha.  Nilikuwa nataka kuota pembe[nilifurahi sana], alikuwa akisoma vizuri sana hata alitamka lafudhi na herufi sahihi haswa, achilia mbali “l” na “r”.  Baada ya swala ya walisoma ziara ya Ashura, na baada yake Sheikh Sawada alianza kuzungumza.

Hii ilikuwa mara yangu ya kwanza kukaa kwenye mimbari ya Mjapani;  Alisema kuhusu Aya ya [tat’hiir] Kutakasa” na kuhusu “mazungumzo” ya Imam Sajjad (as) na mtu huyo wa Syria;  Alisema kuwa mna neema, baraka ambayo hamuithamini kutokana na kughafilika, ukweli ni kwamba kuzaliwa na kukulia katika familia ya kiShia tu ni neema na baraka inayopaswa kushukuriwa.

Alisema kuwa tofauti na mataifa mengine na hata Waislamu wengine, mtaanza kutoka katika sehemu tofauti Siku ya Kiyama, kama mfano wa wakimbiaji ambao wote wanapaswa kuanzia kwenye nukta moja, lakini sisi, kutokana na heshima waliyonayo Ahlul-Bayt[as] na pia wametupa heshima hio,tutaanza kuhesabiwa mbele zaidi ya wengine.

Alisema kwamba, endapo  Mjapani akitaka kufikia hatua muliyopo ni lazima akae miaka 30-40 tena ni kwa uwezo na neema  ya Mungu, miaka 10 lazima asome tauhidi na kupata majibu ya mashaka yake (tena ikiwa ana vitabu  au mtu wa kumuongoza], miaka 10 mingine anahitaji ili kuuelewa na kuukubali utume wa mtume wa mwisho, Nabii Muhammad Mustafa (saww) , na miaka 10 kwa kuelewa  Uimamu na…

Akasema hivi ndivyo baba yake pia alivyo kuwa Muislamu na Mshia.  Ulikuwa mkutano wa kuvutia naye pia alikuwa na maneno matamu na ya kupendeza;  Mwishoni mwa mkusanyiko, tulikuwa wageni kwenye meza ya Aba Abdillah al-Hussein (as) na tukarejea.

 

Hujjat al-Islam Sheikh Ibrahim Sawada

Mazungumzo ya dhati na Sheikh Ibrahim Sawada