Ta’amulat kimeandikwa na Bw. Dk. Abdul-Baqi al-Jazira

Msomi na mwanazuoni mashuhuri wa Kiislamu, Bw. Dk. Abdul-Baqi al-Jazira, alizaliwa nchini Algeria mwaka 1335 Hijria.  Alifanikiwa kupata shahada ya kwanza

katika sayansi ya elimu katika nchi yake.  Mnamo mwaka wa 1407 Hijiria unaolingana na 1365 AH, aliingia katika madhehebu yenye haki ya ushia.  Baada ya kuongozwa, alihamia Iran na huku akipata shahada ya udaktari, alikuwa akijishughulisha na kuandika vitabu vya thamani katika nyanja mbalimbali za kidini na kihistoria, na vilevile alionekana kwenye njia za mitandao kutetea misingi ya itikadi ya Ushia halisi wa Mtume Muhammad[saw] na ameendelea na shughuli hizo hadi sasa.

 Mukhtasari wa maudhui ya kitabu:

Kama jinsi inavyobainika kutokana na jina la kitabu hiki, mwandishi amewaalika wapinzani wa Shia, hususan madhehebu ya Uwahabi, kutafakari na kufikiri.  Amewaalika kwenye changamoto ya kufikiri bila ubaguzi kuhusiana na imani zao katika kitabu hiki, mwandishi ametoa uhakiki wa kielimu na wa wazi wa fikra zisizo sahihi za watu hawa, na pia amejibu baadhi ya mashaka ya kidini ya watu hawa maadui wa Ushia. Kwa mujibu wa mwandishi, kitabu hiki ni mukhtasari wa maswali, ambayo hayakujibiwa kwake kabla ya kua shia, na akaingia Ushia baada ya wanachuoni wa dhehebu yake iliyotangulia kutojibu maswali yake.

Taasisi inapanga kutafsiri na kuchapa kitabu hiki katika lugha ya Kiajemi.