Khossum Al-Hussein – Kilichoandikwa na aliokuwa Mshia Mheshimiwa, Dr. Saleh Alwardani

 

 Muhtasari mfupi wa wasifu wa mwandishi wa kitabu hiki:

Mwanachuoni na msimuliaji mashuhuri wa Kimisri, Bwana Swaleh al-Wardani,alizaliwa mwaka wa 1330 Hijiria, katika mji wa Cairo, Misri, katika familia ya madhehebu

ya ahli sunna na shafii. Mwanzoni mwa miaka yake ya 30 akabadilika kua shia. Mustabsir huyu alifanya shughuli nyingi baada ya kua shia, kiasi ambacho, alitambulika kua kiongozi wa Mashia nchini Misri. Pamoja na kuwepo kwake kwa njia mashuhuri na yenye ufanisi katika mtandao wa kimataifa, alikua na jitihada ya kuchapisha makala za kidini na kisiasa kwenye magazeti na majarida muhimu ya ulimwengu wa Kiislamu. Vilevile aliandika vitabu vingi kuhusu itikadi ya madhehebu ya shia.

Baada ya kua shia, kutokana na uhakika na ukweli wa imani yake, hakuwahi kuwa na hofu yoyote ya kuzieleza waziwazi, na kwa sababu hii, alifungwa jela mara kadhaa na serikali ya Misri kwa shutuma zisizo na msingi.  Pia ameanzisha taasisi ya kitamaduni za dini yenye mbinu ya vyombo vya habari na matangazo ya maandishi, inayoitwa “Dar al-Hadaf”.

 Muhtasari wa yaliyomo katika kitabu hiki:

Mtazamo wa mwandishi katika kuandika kitabu hiki ni kuwatambulisha maadui wa Sayyid al-Shuhadaa (as), tangu mwanzo wa historia ya Kiislamu hadi leo.  Katika kitabu hiki, imethibiti kwamba pamoja na wauaji na madhalimu wa Imam Husein (as) huko nyuma, wafuasi wao wa kifikira na kidini pia walifanya ukatili sawa na ukandamizaji wa watangulizi wao dhidi ya Sayyid al-Shuhada [as].  Anawataja kuwa ni shahidi wake baadhi ya watu kutoka kwa masultani wa dhuluma na wanazuoni wakubwa wa Kisunni na Kiwahabi kama: Ibn Taymiyyah, Albani, Ibn Kathir na wengineo.